Hata hivyo akawatuma manabii, ili kuwarudisha kwa BWANA; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.
Yeremia 25:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi BWANA wa majeshi asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: “Kwa kuwa hamkuyatii maneno yangu, Biblia Habari Njema - BHND “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: “Kwa kuwa hamkuyatii maneno yangu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: “Kwa kuwa hamkuyatii maneno yangu, Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu, Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo bwana Mwenye Nguvu Zote asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu, BIBLIA KISWAHILI Basi BWANA wa majeshi asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu, |
Hata hivyo akawatuma manabii, ili kuwarudisha kwa BWANA; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.
Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosea, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, wasiyasikie maneno yangu.
Mimi nilisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutoitii sauti yangu.
Lakini ninyi hamkunisikiliza, asema BWANA; ili mnikasirishe kwa kazi ya mikono yenu, na kujidhuru nafsi zenu.
angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.
Kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu, asema BWANA, ambayo niliwatuma watumishi wangu, hao manabii, nikiamka mapema, na kuwatuma; lakini hamkutaka kusikiliza, asema BWANA.
Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, BWANA wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunitii, asema BWANA.