Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Yeremia 25:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia, wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka. Biblia Habari Njema - BHND Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia, wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia, wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka. Neno: Bibilia Takatifu Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia, viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea. Neno: Maandiko Matakatifu Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia, viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea. BIBLIA KISWAHILI Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka. |
Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, lakini sitawasikiliza.
Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kuomboleza kwao walio hodari katika kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao.
tena, Sedekia, mfalme wa Yuda, hatapona kutoka katika mikono ya Wakaldayo, lakini hakika yake atatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli, atanena naye ana kwa ana, na watatazamana macho kwa macho;
tena wewe hutaokoka mkononi mwake, lakini hakika utakamatwa, na kutiwa katika mikono yake; na utatazamana macho kwa macho na mfalme wa Babeli, naye atasema nawe mdomo kwa mdomo, nawe utakwenda Babeli.
ndipo Sedekia, mfalme, akatuma watu wamlete; naye mfalme akamwuliza kwa siri ndani ya nyumba yake, akasema, Je! Liko neno lililotoka kwa BWANA? Yeremia akasema, Liko. Akasema pia, Utatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli.
bali ukikataa kutoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi, mji huu utatiwa katika mikono ya Wakaldayo nao watauteketeza, hata na wewe hutajiepusha na mikono yao.
Na watawatoa wake zako, na watoto wako wote, na kuwachukua kwa Wakaldayo; wala wewe hutapona na mikono yao, bali utakamatwa kwa mkono wa mfalme wa Babeli, nawe utakuwa sababu ya kuteketezwa mji huu.
Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA.
Lakini alimwasi kwa kutuma wajumbe huko Misri, wampe farasi na watu wengi. Je! Atafanikiwa? Afanyaye mambo hayo ataokoka? Atalivunja agano, kisha akaokoka?
Kwa maana amekidharau kiapo kwa kulivunja agano; na tazama, ametia mkono wake, na pamoja na hayo ameyatenda mambo hayo yote; hataokoka.
Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;