Wakati ule watumishi wa Nebukadneza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa.
Yeremia 24:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akanionesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la BWANA, baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babuloni kuwahamisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wa Yuda, mafundi stadi na masonara, kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babuloni, Mwenyezi-Mungu alinionesha ono hili: Niliona vikapu viwili vya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babuloni kuwahamisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wa Yuda, mafundi stadi na masonara, kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babuloni, Mwenyezi-Mungu alinionesha ono hili: Niliona vikapu viwili vya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babuloni kuwahamisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wa Yuda, mafundi stadi na masonara, kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babuloni, Mwenyezi-Mungu alinionesha ono hili: Niliona vikapu viwili vya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli na Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Mwenyezi Mungu akanionesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli, bwana akanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la bwana. BIBLIA KISWAHILI BWANA akanionesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la BWANA, baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli. |
Wakati ule watumishi wa Nebukadneza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa.
Mwaka ulipokwisha, Nebukadneza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
Miji ya Negebu imefungwa malango yake, wala hapana mtu wa kuyafungua; Yuda amechukuliwa mateka; amechukuliwa kabisa mateka.
ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hakuvichukua, hapo alipomchukua Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu mpaka Babeli, pamoja na wakuu wote wa Yuda, na Yerusalemu;
Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema BWANA; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.
Maneno haya ndiyo maneno ya barua, ambayo nabii Yeremia alituma toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadneza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hadi Babeli;
(hapo walipokwisha kutoka Yerusalemu Yekonia mfalme, na mama yake mfalme, na matowashi, na wakuu wa Yuda na Yerusalemu, na mafundi, na wahunzi;)
Na Sedekia, mwana wa Yosia, akamiliki baada ya Konia, mwana wa Yehoyakimu, ambaye Nebukadneza amemfanya mtawala katika nchi ya Yuda.
akakikata kitawi kilicho juu katika vitawi vyake, akakichukua mpaka nchi ya biashara, akakiweka katika mji wa wachuuzi.
Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu ya milima ya Israeli.
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.
Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukaviteketeza vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.
Haya ndiyo aliyonionesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake.
Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kulia ili kushindana naye.