Na Sedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, BWANA asema hivi, Kwa hizo utawasukuma Washami, hata waharibike.
Yeremia 23:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, mimi niko juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli mimi Mwenyezi-Mungu nasema, nitawashambulia manabii wanaoropoka maneno yao wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi-Mungu asema’. Biblia Habari Njema - BHND Kweli mimi Mwenyezi-Mungu nasema, nitawashambulia manabii wanaoropoka maneno yao wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi-Mungu asema’. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli mimi Mwenyezi-Mungu nasema, nitawashambulia manabii wanaoropoka maneno yao wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi-Mungu asema’. Neno: Bibilia Takatifu “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotumia ndimi zao wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi Mungu asema.’ Neno: Maandiko Matakatifu “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘bwana asema.’ BIBLIA KISWAHILI Tazama, mimi niko juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, |
Na Sedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, BWANA asema hivi, Kwa hizo utawasukuma Washami, hata waharibike.
Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya manabii, watu mia nne; akawaambia, Je! Tuende Ramoth-gileadi vitani, au niache? Wakasema, Kwea; kwa kuwa Mungu atautia mkononi mwa mfalme.
wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wowote.
Basi kwa sababu hiyo mimi niko juu ya manabii hao, asema BWANA, wanaompokonya kila mtu jirani yake maneno yangu.
Tazama, mimi niko juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.
Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; BWANA hakukutuma; lakini unawapa tumaini watu hawa kwa maneno ya uongo.
Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa.
Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.