Yeremia 22:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini nchi ile ambayo wanatamani kuirudia, hawatairudia kamwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtatamani kwa hamu kubwa kurudi katika nchi hii, lakini hamtarudi kamwe. Biblia Habari Njema - BHND Mtatamani kwa hamu kubwa kurudi katika nchi hii, lakini hamtarudi kamwe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtatamani kwa hamu kubwa kurudi katika nchi hii, lakini hamtarudi kamwe. Neno: Bibilia Takatifu Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” Neno: Maandiko Matakatifu Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” BIBLIA KISWAHILI Lakini nchi ile ambayo wanatamani kuirudia, hawatairudia kamwe. |
Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee, Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali; Kwa maana yeye hatarudi tena, Wala hataiona nchi aliyozaliwa.
Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za Shalumu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; aliyemiliki badala ya Yosia, baba yake, yeye aliyetoka mahali hapa; Hatarudi huku tena;
bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe.
Nami nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende katika nchi nyingine ambayo hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko.
Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua?
Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema BWANA; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.
Maana BWANA wa majeshi Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama hasira yangu, na ghadhabu yangu, ilivyomwagwa juu ya hao wakaao Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu, mtakapoingia Misri; nanyi mtakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu; wala hamtapaona mahali hapa tena.
hata katika watu wale wa Yuda waliosalia, waliokwenda nchi ya Misri ili wakae huko, hapatakuwa na mtu yeyote atakayepona, wala atakayesalia, na kupata kurudi nchi ya Yuda, ambayo wanatamani kurudi ili kukaa huko; maana hapana atakayerudi, ila wao watakaopona.