Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yeremia 20:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini nikisema, “Sitamtaja Mwenyezi-Mungu, wala sitasema tena kwa jina lake,” moyoni mwangu huwa na kitu kama moto uwakao, uliofungiwa ndani ya mifupa yangu. Najaribu sana kuuzuia humo, lakini ninashindwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini nikisema, “Sitamtaja Mwenyezi-Mungu, wala sitasema tena kwa jina lake,” moyoni mwangu huwa na kitu kama moto uwakao, uliofungiwa ndani ya mifupa yangu. Najaribu sana kuuzuia humo, lakini ninashindwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini nikisema, “Sitamtaja Mwenyezi-Mungu, wala sitasema tena kwa jina lake,” moyoni mwangu huwa na kitu kama moto uwakao, uliofungiwa ndani ya mifupa yangu. Najaribu sana kuuzuia humo, lakini ninashindwa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Lakini nikisema, “Sitamtaja wala kusema tena kwa jina lake,” neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto, moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu. Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu; kweli, siwezi kujizuia.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Lakini kama nikisema, “Sitamtaja wala kusema tena kwa jina lake,” neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto, moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu. Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu; kweli, siwezi kujizuia.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yeremia 20:9
21 Marejeleo ya Msalaba  

Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka; Nilisema kwa ulimi wangu,

Je! Neno langu si kama moto? Asema BWANA; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?

Kuhusu habari za manabii. Moyo wangu ndani yangu umevunjika, Mifupa yangu yote inatikisika. Nimekuwa kama mtu aliye mlevi, Na kama mtu aliyeshindwa na divai; kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.

Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.

Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.

Basi roho ikaniinua, ikanichukua mahali pengine; nami nikaenda kwa uchungu, na hasira kali rohoni mwangu, na mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu kwa nguvu.

Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.

Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?

Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.

Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akateremka hadi Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akalipa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.

Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.

Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.

Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.

maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.