Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 19:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

BWANA akasema hivi, Nenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kwa mfinyanzi. Kisha, wachukue baadhi ya wazee wa watu na baadhi ya makuhani viongozi,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kwa mfinyanzi. Kisha, wachukue baadhi ya wazee wa watu na baadhi ya makuhani viongozi,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kwa mfinyanzi. Kisha, wachukue baadhi ya wazee wa watu na baadhi ya makuhani viongozi,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hili ndilo asemalo bwana: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

BWANA akasema hivi, Nenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 19:1
20 Marejeleo ya Msalaba  

Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.


Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.


BWANA akaniambia hivi, Nenda ukajinunulie kitambaa cha kitani, ukajifunge kiunoni, wala usikitie majini.


Ndipo watu kadhaa miongoni mwa wazee wa nchi wakaondoka, wakanena na mkutano wa watu, wakisema,


BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Twaa hati hizi, hati hii ya kununua, hati hii iliyopigwa mhuri, na hii iliyo wazi pia, ukazitie katika chombo cha udongo, zipate kukaa siku nyingi.


Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mikono ya mfinyanzi!


Wewe nawe, mwanadamu, jipatie tofali uliweke mbele yako, kisha, chora juu yake mfano wa mji, yaani, Yerusalemu;


Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.


Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.


Kisha BWANA akamwambia Musa, Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa Israeli, ambao wewe unawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na viongozi juu yao; ukawalete katika hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe.


Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;


Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;


Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.


Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.