wakati huo BWANA alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.
Yeremia 18:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha maneno yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yeremia, inuka uende nyumbani kwa mfinyanzi, na huko nitakupa maneno yangu.” Biblia Habari Njema - BHND “Yeremia, inuka uende nyumbani kwa mfinyanzi, na huko nitakupa maneno yangu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yeremia, inuka uende nyumbani kwa mfinyanzi, na huko nitakupa maneno yangu.” Neno: Bibilia Takatifu “Shuka uende hadi nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” Neno: Maandiko Matakatifu “Shuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” BIBLIA KISWAHILI Ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha maneno yangu. |
wakati huo BWANA alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.
BWANA akaniambia hivi, Nenda ukajinunulie kitambaa cha kitani, ukajifunge kiunoni, wala usikitie majini.
Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na tazama, alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu.
Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao.
Haya ndiyo aliyonionesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake.
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,