Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
Yeremia 17:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya maji, upenyezao mizizi yake karibu na chemchemi. Hauogopi wakati wa joto ufikapo, majani yake hubaki mabichi. Hauhangaiki katika mwaka wa ukame, na hautaacha kuzaa matunda. Biblia Habari Njema - BHND Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya maji, upenyezao mizizi yake karibu na chemchemi. Hauogopi wakati wa joto ufikapo, majani yake hubaki mabichi. Hauhangaiki katika mwaka wa ukame, na hautaacha kuzaa matunda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya maji, upenyezao mizizi yake karibu na chemchemi. Hauogopi wakati wa joto ufikapo, majani yake hubaki mabichi. Hauhangaiki katika mwaka wa ukame, na hautaacha kuzaa matunda. Neno: Bibilia Takatifu Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji. Hauogopi wakati wa joto ujapo; majani yake ni mabichi daima. Hauna hofu katika mwaka wa ukame na hautaacha kuzaa matunda.” Neno: Maandiko Matakatifu Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji. Hauogopi wakati wa joto ujapo; majani yake ni mabichi daima. Hauna hofu katika mwaka wa ukame na hautaacha kuzaa matunda.” BIBLIA KISWAHILI Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. |
Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Kwa maana ni yakini, nitakuokoa, wala hutaanguka kwa upanga, lakini nafsi yako itakuwa kama nyara kwako; kwa kuwa ulinitumaini mimi, asema BWANA.
Tazama, Mwashuri alikuwa mwerezi katika Lebanoni, wenye matawi mazuri, na kifuniko chenye uvuli, na kimo kirefu; na kilele chake kilikuwa kati ya matawi mapana.
Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.