Basi yule afisa, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Yeremia 17:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyo ni kama kichaka jangwani, hataona chochote chema kikimjia. Ataishi mahali pakavu nyikani, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Biblia Habari Njema - BHND Huyo ni kama kichaka jangwani, hataona chochote chema kikimjia. Ataishi mahali pakavu nyikani, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyo ni kama kichaka jangwani, hataona chochote chema kikimjia. Ataishi mahali pakavu nyikani, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Neno: Bibilia Takatifu Atakuwa kama kichaka cha jangwani; hataona mafanikio yatakapokuja. Ataishi katika sehemu zisizo na maji, katika nchi ya chumvi ambapo hakuna yeyote aishiye humo. Neno: Maandiko Matakatifu Atakuwa kama kichaka cha jangwani; hataona mafanikio yatakapokuja. Ataishi katika sehemu zisizo na maji, katika nchi ya chumvi ambapo hakuna yeyote aishiye humo. BIBLIA KISWAHILI Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. |
Basi yule afisa, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Hata wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakastawi. Mwishowe wataangamizwa milele;
basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Shemaya, Mnehelami, na wazawa wake; hatakuwa na mtu atakayekaa katika watu hawa, wala hatayaona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA; kwa sababu amenena maneno ya uasi juu ya BWANA.
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;
Abimeleki akapigana na huo mji mchana kutwa; akautwaa mji, akawaua watu waliokuwamo ndani yake; kisha akauteketeza mji, na kuutia chumvi.