Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.
Yeremia 17:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, wao waniambia, Neno la BWANA liko wapi? Na lije, basi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama watu wanavyoniambia: “Jambo alilotishia Mwenyezi-Mungu liko wapi? Acha basi lije!” Biblia Habari Njema - BHND Tazama watu wanavyoniambia: “Jambo alilotishia Mwenyezi-Mungu liko wapi? Acha basi lije!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama watu wanavyoniambia: “Jambo alilotishia Mwenyezi-Mungu liko wapi? Acha basi lije!” Neno: Bibilia Takatifu Wao huendelea kuniambia, “Liko wapi neno la Mwenyezi Mungu? Sasa na litimie!” Neno: Maandiko Matakatifu Wao huendelea kuniambia, “Liko wapi neno la bwana? Sasa na litimie!” BIBLIA KISWAHILI Tazama, wao waniambia, Neno la BWANA liko wapi? Na lije, basi. |
Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.
Mwanadamu, ni mithali gani hii mliyo nayo katika nchi ya Israeli, mkisema, Siku hizo zinakawia na maono yote hayatimizwi.
Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwa nini kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.
Mmemchokesha BWANA kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye haki yuko wapi?