Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Yeremia 16:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe hutaoa mke, wala hutakuwa na wana wala binti mahali hapa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wewe hutaoa wala hutapata watoto mahali hapa. Biblia Habari Njema - BHND “Wewe hutaoa wala hutapata watoto mahali hapa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wewe hutaoa wala hutapata watoto mahali hapa. Neno: Bibilia Takatifu “Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.” Neno: Maandiko Matakatifu “Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.” BIBLIA KISWAHILI Wewe hutaoa mke, wala hutakuwa na wana wala binti mahali hapa. |
Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za wana, na kuhusu habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na kuhusu habari za mama zao waliowazaa, na kuhusu habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;
oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini; Hofu zangu zije pande zote; Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusalia Katika siku ya hasira ya BWANA; Hao niliowabeba na kuwalea Huyo adui yangu amewakomesha.
Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
Kwa maana tazama, siku zitakuja watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha.