Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 15:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nami nimewapepea kwa kipepeo katika malango ya nchi nimewaondolea watoto wao, nimewaharibu watu wangu; hata hivyo hawakurudi na kuziacha njia zao.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nimewapepeta kwa chombo cha kupuria, katika kila mji nchini; nimewaangamiza watu wangu, kwa kuwaulia mbali watoto wao, lakini hawakuacha njia zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nimewapepeta kwa chombo cha kupuria, katika kila mji nchini; nimewaangamiza watu wangu, kwa kuwaulia mbali watoto wao, lakini hawakuacha njia zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nimewapepeta kwa chombo cha kupuria, katika kila mji nchini; nimewaangamiza watu wangu, kwa kuwaulia mbali watoto wao, lakini hawakuacha njia zao.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nitawapepeta kwa ungo kwenye malango ya miji ya nchi. Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu, kwa maana hawajabadili njia zao.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nitawapepeta kwa uma wa kupepetea kwenye malango ya miji katika nchi. Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu, kwa maana hawajabadili njia zao.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nami nimewapepea kwa kipepeo katika malango ya nchi nimewaondolea watoto wao, nimewaharibu watu wangu; hata hivyo hawakurudi na kuziacha njia zao.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 15:7
21 Marejeleo ya Msalaba  

Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.


Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia BWANA, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli.


Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Lakini watu hao hawakumwelekea yeye aliyewapiga, wala kumtafuta BWANA wa majeshi.


Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.


Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.


Nami nitawatuma wapepetaji watakaompepea mpaka Babeli, nao wataifanya nchi yake kuwa tupu; kwa kuwa katika siku ya taabu watakuwa juu yake pande zote.


Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu.


Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.


Nawe, mwanadamu, je! Haitakuwa hivi katika siku hiyo nitakapowaondolea nguvu zao, na furaha ya utukufu wao, na kilichotamaniwa na macho yao, ambacho walikiinulia mioyo yao, watoto wao wa kiume na watoto wao wa kike,


Naam, nitaleta watu watembee juu yenu, naam, watu wangu Israeli; nao watakumiliki, nawe utakuwa urithi wao, wala hutawaua watoto wao tena tangu leo.


Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, BWANA wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunitii, asema BWANA.


Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.


Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.


Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.


Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.