Yeremia 15:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ni nani atakayekuhurumia, Ee Yerusalemu? Au ni nani atakayekulilia? Au ni nani atakayegeuka upande ili kuuliza habari za hali yako? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Ni nani atakayewahurumia, enyi watu wa Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza juu yenu? Nani atasimama kuuliza habari zenu? Biblia Habari Njema - BHND “Ni nani atakayewahurumia, enyi watu wa Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza juu yenu? Nani atasimama kuuliza habari zenu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Ni nani atakayewahurumia, enyi watu wa Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza juu yenu? Nani atasimama kuuliza habari zenu? Neno: Bibilia Takatifu “Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? Ni nani atakayesimama ili kuuliza kuhusu hali yako? Neno: Maandiko Matakatifu “Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? Ni nani atakayesimama ili kuuliza kuhusu hali yako? BIBLIA KISWAHILI Maana ni nani atakayekuhurumia, Ee Yerusalemu? Au ni nani atakayekulilia? Au ni nani atakayegeuka upande ili kuuliza habari za hali yako? |
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani.
Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza?
Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.
Maana BWANA asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema BWANA, hata fadhili zangu na rehema zangu.
Na baada ya hayo, asema BWANA, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu.
Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; BWANA ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji?
Basi wakageuka wakaenda kuko, wakafika katika nyumba ya huyo kijana Mlawi, huko nyumbani kwa Mika, kumwamkia.
Basi Daudi akaviacha vile vyombo vyake katika mkono wa mlinda vyombo, akalikimbilia jeshi, akafika, akawasalimu ndugu zake.
Daudi akatuma vijana kumi, Daudi naye akawaambia hao vijana, Kweeni mwende Karmeli, na kumwendea huyu Nabali ili mkampe salamu zangu;