Yeremia 15:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mbele ya watu hawa, nitakufanya ukuta imara wa shaba. Watapigana nawe, lakini hawataweza kukushinda, maana, mimi niko pamoja nawe, kukuokoa na kukukomboa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema - BHND Mbele ya watu hawa, nitakufanya ukuta imara wa shaba. Watapigana nawe, lakini hawataweza kukushinda, maana, mimi niko pamoja nawe, kukuokoa na kukukomboa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mbele ya watu hawa, nitakufanya ukuta imara wa shaba. Watapigana nawe, lakini hawataweza kukushinda, maana, mimi niko pamoja nawe, kukuokoa na kukukomboa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Neno: Bibilia Takatifu Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa, ngome ya ukuta wa shaba; watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa maana mimi niko pamoja nawe kukuponya na kukuokoa,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa, ngome ya ukuta wa shaba; watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa maana mimi niko pamoja nawe kukuponya na kukuokoa,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA. |
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto wa kiume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.
Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.
Basi Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamwagiza Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, katika habari za Yeremia, akisema,
Msimwogope mfalme wa Babeli, mnayemwogopa; msimwogope, asema BWANA; maana mimi ni pamoja nanyi, niwaokoe, na kuwaponya kutoka kwa mkono wake.
Tazama, nimeufanya uso wako kuwa mgumu juu ya nyuso zao, na kipaji cha uso chako kuwa kigumu juu ya vipaji vya nyuso zao.
Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi.
Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuri liwakalo moto; naye atatuokoa mkononi mwako, Ee mfalme.