Hata kwake pia utatoka, na mikono yako juu ya kichwa chako; kwa maana BWANA amewakataa uliowakimbilia, wala hutafanikiwa katika hao.
Yeremia 14:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa sababu ya nchi iliyopasuka, Kwa kuwa mvua haikunyesha katika nchi, Wakulima wametahayarika, Na kuvifunika vichwa vyao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakulima wanahuzunika na kufunika vichwa vyao kwa kuona jinsi ardhi ilivyonyauka. Biblia Habari Njema - BHND Wakulima wanahuzunika na kufunika vichwa vyao kwa kuona jinsi ardhi ilivyonyauka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakulima wanahuzunika na kufunika vichwa vyao kwa kuona jinsi ardhi ilivyonyauka. Neno: Bibilia Takatifu Ardhi imepasuka nyufa kwa sababu hakuna mvua katika nchi; wakulima wana hofu na wanafunika vichwa vyao. Neno: Maandiko Matakatifu Ardhi imepasuka nyufa kwa sababu hakuna mvua katika nchi; wakulima wana hofu na wanafunika vichwa vyao. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu ya nchi iliyopasuka, Kwa kuwa mvua haikunyesha katika nchi, Wakulima wametahayarika, Na kuvifunika vichwa vyao. |
Hata kwake pia utatoka, na mikono yako juu ya kichwa chako; kwa maana BWANA amewakataa uliowakimbilia, wala hutafanikiwa katika hao.
Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika.
Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; mabohari yameachwa ukiwa; ghala zimeharibika; kwa maana nafaka imekauka.
Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.
Basi kutoka miji miwili mitatu walitangatanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;