basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
Yeremia 14:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye BWANA akaniambia, Usiwaombee watu hawa wapate heri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Usiwaombee watu hawa fanaka. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Usiwaombee watu hawa fanaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Usiwaombee watu hawa fanaka. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. BIBLIA KISWAHILI Naye BWANA akaniambia, Usiwaombee watu hawa wapate heri. |
basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
Basi, usiwaombee watu hawa, wala usipaze sauti yako, wala kuwaombea dua watu hawa; maana sitawasikia wakati watakaponililia kwa ajili ya taabu yao.
Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.
Basi, wewe usiwaombee watu hawa, wala usiwapazie sauti yako, wala kuwaombea dua, wala usinisihi kwa ajili yao; kwa maana sitakusikiliza.
Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.