Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Yeremia 13:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikakitwaa kile kitambaa katika mahali pale nilipokificha; na tazama, kitambaa kilikuwa kimeharibika, hakikufaa tena kwa lolote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nikaenda kwenye mto Eufrate, nikachimbua na kukitoa kile kikoi mahali nilipokuwa nimekificha. Nilipokitoa, nilishangaa kukiona kuwa kilikuwa kimeharibika kabisa; kilikuwa hakifai tena. Biblia Habari Njema - BHND Basi, nikaenda kwenye mto Eufrate, nikachimbua na kukitoa kile kikoi mahali nilipokuwa nimekificha. Nilipokitoa, nilishangaa kukiona kuwa kilikuwa kimeharibika kabisa; kilikuwa hakifai tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nikaenda kwenye mto Eufrate, nikachimbua na kukitoa kile kikoi mahali nilipokuwa nimekificha. Nilipokitoa, nilishangaa kukiona kuwa kilikuwa kimeharibika kabisa; kilikuwa hakifai tena. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa. BIBLIA KISWAHILI Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikakitwaa kile kitambaa katika mahali pale nilipokificha; na tazama, kitambaa kilikuwa kimeharibika, hakikufaa tena kwa lolote. |
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyo yao, na kufuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, watakuwa hali moja na kitambaa hiki kisichofaa kwa lolote.
Hata ikawa, baada ya siku nyingi, BWANA akaniambia, Ondoka, nenda mpaka mto Frati, ukakitwae kile kitambaa, nilichokuamuru kukificha huko.