katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.
Yeremia 12:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wateule wangu wamenigeuka, wamekuwa kama simba porini, wameningurumia mimi; ndiyo maana nawachukia. Biblia Habari Njema - BHND Wateule wangu wamenigeuka, wamekuwa kama simba porini, wameningurumia mimi; ndiyo maana nawachukia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wateule wangu wamenigeuka, wamekuwa kama simba porini, wameningurumia mimi; ndiyo maana nawachukia. Neno: Bibilia Takatifu Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba wa msituni. Nauchukia kwa kuwa unaningurumia. Neno: Maandiko Matakatifu Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba wa msituni. Huningurumia mimi, kwa hiyo ninamchukia. BIBLIA KISWAHILI Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia. |
katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.
Wanasimba wamenguruma juu yake, wametoa sana sauti zao; Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketea, haina watu.
Basi alipoendelea na ukahaba wake waziwazi, na kufunua uchi wake; ndipo roho yangu ikafarakana naye, kama ilivyofarakana na dada yake.
Uovu wao wote u katika Gilgali; maana huko niliwachukia; kwa sababu ya uovu wa matendo yao nitawafukuza watoke katika nyumba yangu; sitawapenda tena; wakuu wao wote ni waasi.
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.
Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mnawapokonya joho lililo juu ya nguo za hao wapitao salama bila kutarajia vita.
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.