Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Yeremia 12:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa katika nchi ya amani uko salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu asema, “Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka, utawezaje kushindana na farasi? Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi, utafanyaje katika msitu wa Yordani? Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu asema, “Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka, utawezaje kushindana na farasi? Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi, utafanyaje katika msitu wa Yordani? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu asema, “Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka, utawezaje kushindana na farasi? Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi, utafanyaje katika msitu wa Yordani? Neno: Bibilia Takatifu “Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda, unawezaje kushindana na farasi? Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama, utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani? Neno: Maandiko Matakatifu “Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda, unawezaje kushindana na farasi? Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama, utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani? BIBLIA KISWAHILI Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa katika nchi ya amani uko salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani? |
Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maporomoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la BWANA, usije ukafa kwa mkono wetu.
Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote BWANA aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa.
Mfalme akamwamuru Yerameeli, mwana wa mfalme, na Seraya, mwana wa Azrieli, na Shelemia, mwana wa Abdeeli, wamkamate Baruku, mwandishi, na Yeremia, nabii; lakini BWANA aliwaficha.
Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno),
Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.