La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Yeremia 12:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi? Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi? Neno: Bibilia Takatifu Wewe daima u mwenye haki, Ee Mwenyezi Mungu, niletapo mashtaka mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasio waaminifu wote wanaishi salama? Neno: Maandiko Matakatifu Wewe daima u mwenye haki, Ee bwana, niletapo mashtaka mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasio waaminifu wote wanaishi kwa raha? BIBLIA KISWAHILI Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama? |
La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Ee BWANA, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.
Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyo kweli, lakini sisi tumetenda yaliyo maovu;
Hema za wanyang'anyi hufanikiwa, Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama; Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.
Watu huugua toka mji ulio na watu wengi, Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele; Wala Mungu hauangalii upumbavu.
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Hata wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakastawi. Mwishowe wataangamizwa milele;
Kuna ubatili unaofanyika juu ya nchi, kwamba wako wenye haki nao wapatilizwa kama kwa kazi yao waovu; tena wako waovu, nao wapatilizwa kama kwa kazi yao wenye haki. Nami nikasema ya kuwa hayo nayo ni ubatili.
Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.
Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye fikira na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila; naam, wamepiga kelele nyuma yako; usiwasadiki, wajapokuambia maneno mazuri.
Bali, kama vile mke amwachavyo mumewe kwa hiana, ndivyo mlivyonitenda mimi kwa hiana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA.
Nami nilisema baada ya yeye kuyatenda hayo yote, Atanirudia mimi, lakini hakurudi; na dada yake, Yuda mwenye hiana, akayaona hayo.
Hata nikiisha kumpa Baruku, mwana wa Neria, hati ile ya kununua, nilimwomba BWANA, nikisema,
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.
Lakini ninyi mwasema, Njia ya Bwana si sawa. Sikilizeni sasa, Enyi nyumba ya Israeli; Je! Njia yangu siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa?
Basi BWANA anayachungulia mabaya hayo, akatuletea; maana BWANA, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti yake.
Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna aibu, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.
Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu inayotolewa huwa imepotoshwa.
BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.
Mmemchokesha BWANA kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye haki yuko wapi?
Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.