Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 11:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Naye BWANA akaniambia, Fitina imeonekana katika watu wa Yuda, na katika wenyeji wa Yerusalemu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Tena Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu wanafanya njama za kuniasi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Tena Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu wanafanya njama za kuniasi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Tena Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu wanafanya njama za kuniasi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Kuna fitina inayoendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kisha bwana akaniambia, “Kuna shauri baya linaloendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Naye BWANA akaniambia, Fitina imeonekana katika watu wa Yuda, na katika wenyeji wa Yerusalemu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 11:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.


Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; maana kila mmoja wao, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa, ni mtamanifu; tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.


Na kama vile makundi ya wanyang'anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana.


Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.


akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.


Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.