Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yeremia 11:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Tena BWANA akanijulisha haya, nami nikayajua; ndipo uliponionesha matendo yao.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu alinijulisha, nami nikaelewa; Mwenyezi-Mungu alinijulisha njama zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu alinijulisha, nami nikaelewa; Mwenyezi-Mungu alinijulisha njama zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu alinijulisha, nami nikaelewa; Mwenyezi-Mungu alinijulisha njama zao.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa sababu Mwenyezi Mungu alinifunulia na kunionesha hila zao mbaya, na waliyokuwa wanayafanya niliyafahamu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa sababu bwana alinifunulia hila zao mbaya, nilizifahamu, kwa kuwa wakati ule alinionyesha yale waliyokuwa wanayafanya.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tena BWANA akanijulisha haya, nami nikayajua; ndipo uliponionesha matendo yao.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yeremia 11:18
8 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Elisha alikuwa akikaa nyumbani mwake, na wazee wakikaa pamoja naye; na mfalme akamtuma mtu wa mbele yake; lakini hata kabla ya kufika kwake yule aliyetumwa, akawaambia wazee, Je! Mwaona jinsi huyu mwana wa mwuaji alivyotuma aniondolee kichwa changu? Angalieni, huyo aliyetumwa akifika, fungeni mlango, mkamzuie mlangoni; je! Sauti ya miguu ya bwana wake haiko nyuma yake?


Lakini mimi nilikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.


Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; naye atawatuma mara moja.


Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?