hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
Yeremia 10:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake. Biblia Habari Njema - BHND Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake. Neno: Bibilia Takatifu Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. Hupeleka miali ya radi pamoja na mvua, naye huuleta upepo kutoka ghala zake. Neno: Maandiko Matakatifu Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua, naye huuleta upepo kutoka ghala zake. BIBLIA KISWAHILI Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake. |
hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.
BWANA alinguruma kutoka mbinguni, Yeye Aliye Juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto.
Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; na BWANA akaleta ngurumo na mvua ya mawe, na moto ukashuka juu ya nchi; BWANA akanyesha mvua ya mawe juu ya nchi yote ya Misri.
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema BWANA, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi;
Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea majuma ya mavuno yaliyoamriwa.
Atoapo sauti yake pana kishindo cha maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.
Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.