Yakobo 4:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi. Biblia Habari Njema - BHND Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi. Neno: Bibilia Takatifu Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi. Neno: Maandiko Matakatifu Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi. BIBLIA KISWAHILI Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. |
Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana kisingizio kwa dhambi yao.
Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini kwa kuwa sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.
ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? La hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.
Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.