Yakobo 3:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani. Biblia Habari Njema - BHND Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani. Neno: Bibilia Takatifu Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. Neno: Maandiko Matakatifu Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. BIBLIA KISWAHILI Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. |
Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.
Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu;
Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja.
Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoeshwa nayo matunda ya haki yenye amani.