Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Yakobo 2:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa. Biblia Habari Njema - BHND Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa. Neno: Bibilia Takatifu Vivyo hivyo, imani peke yake, kama haikuambatana na matendo, imekufa. Neno: Maandiko Matakatifu Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa. BIBLIA KISWAHILI Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. |
Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na subira yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.
Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.
Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?