Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.
Wimbo Ulio Bora 4:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Umenishangaza moyo, dada yangu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, Kwa mtupo mmoja wa macho yako, Kwa mkufu mmoja wa shingo yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umefurahisha moyo wangu, dada yangu, bi arusi, umefurahisha moyo wangu, kwa kunitupia jicho mara moja tu, na kwa huo mkufu wako shingoni. Biblia Habari Njema - BHND Umefurahisha moyo wangu, dada yangu, bi arusi, umefurahisha moyo wangu, kwa kunitupia jicho mara moja tu, na kwa huo mkufu wako shingoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umefurahisha moyo wangu, dada yangu, bi arusi, umefurahisha moyo wangu, kwa kunitupia jicho mara moja tu, na kwa huo mkufu wako shingoni. Neno: Bibilia Takatifu Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeiba moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeiba moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako. BIBLIA KISWAHILI Umenishangaza moyo, dada yangu, Bibi harusi, umenishangaza moyo, Kwa mtupo mmoja wa macho yako, Kwa mkufu mmoja wa shingo yako. |
Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.
Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Binti za wafalme wamo Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki. Katika mkono wako wa kulia amesimama malkia Akiwa amevaa dhahabu safi ya Ofiri.
Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.
Jinsi pendo lako lilivyo nzuri, dada yangu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.
Bustani iliyofungwa ni dada yangu, bibi arusi, Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa mhuri.
Uyageuzie macho yako mbali nami, Kwa maana yamenitisha sana. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.
Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.
Kwa maana yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye kaka yangu, na dada yangu na mama yangu.
Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.
Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa niliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.