Ikawa tokea wakati huo, nusu ya watumishi wangu walitumika katika kazi hiyo, na nusu yao wakaishika mikuki, na ngao, na pinde, na darii; na viongozi walikuwa nyuma ya nyumba yote ya Yuda.
Wimbo Ulio Bora 3:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mmoja wao ameshika upanga, kila mmoja wao ni hodari wa vita. Kila mmoja ana upanga wake mkononi, tayari kumkabili adui usiku. Biblia Habari Njema - BHND Kila mmoja wao ameshika upanga, kila mmoja wao ni hodari wa vita. Kila mmoja ana upanga wake mkononi, tayari kumkabili adui usiku. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mmoja wao ameshika upanga, kila mmoja wao ni hodari wa vita. Kila mmoja ana upanga wake mkononi, tayari kumkabili adui usiku. Neno: Bibilia Takatifu wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya vitisho vya usiku. Neno: Maandiko Matakatifu wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku. BIBLIA KISWAHILI Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku. |
Ikawa tokea wakati huo, nusu ya watumishi wangu walitumika katika kazi hiyo, na nusu yao wakaishika mikuki, na ngao, na pinde, na darii; na viongozi walikuwa nyuma ya nyumba yote ya Yuda.
Watu wale walioujenga ukuta, na wale waliochukua mizigo, walijitweka wenyewe, kila mtu alifanya kazi kwa mkono mmoja, na kwa mkono wake wa pili alishika silaha yake;
Mimi, BWANA, nililinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.
Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kulia.