Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme.
Wimbo Ulio Bora 3:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama! Ni machela ya Solomoni; amebebwa juu ya kiti chake cha enzi; amezungukwa na walinzi sitini, mashujaa bora wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Tazama! Ni machela ya Solomoni; amebebwa juu ya kiti chake cha enzi; amezungukwa na walinzi sitini, mashujaa bora wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama! ni machela ya Solomoni; amebebwa juu ya kiti chake cha enzi; amezungukwa na walinzi sitini, mashujaa bora wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Tazama! Ni gari la Sulemani likisindikizwa na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli, Neno: Maandiko Matakatifu Tazama! Ni gari la Sulemani lisindikizwalo na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli, BIBLIA KISWAHILI Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli. |
Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme.
Lakini kwa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu yeyote shokoa; ila wao walikuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maafisa wake, makamanda wa magari yake na wapanda farasi wake.
Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
Basi, nikaweka watu, mahali pa chini pa nafasi iliyokuwa nyuma ya ukuta, mahali palipokuwa wazi, kwa kadiri ya jamaa zao, nikawaweka waliojihami na panga zao, na mikuki yao, na pinde zao.
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku.
Tena, kulikuwa na vita kali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu yeyote aliyekuwa hodari, au mtu yeyote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.
Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinzi wangu binafsi daima.
Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe wenu walio wazuri sana, na punda wenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe.