Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
Wimbo Ulio Bora 3:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu, kama walivyo paa au swala, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika. Biblia Habari Njema - BHND Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu, kama walivyo paa au swala, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu, kama walivyo paa au swala, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika. Neno: Bibilia Takatifu Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe. BIBLIA KISWAHILI Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. |
Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani.
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Msiyachochee mapenzi, au kuyaamsha, Hadi yatakapokuwa tayari.
Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.