Wimbo Ulio Bora 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kitambo kidogo tu nilipoachana nao, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mara tu nilipoachana nao, nilimwona mpenzi wangu wa moyo; nikamshika wala sikumwachia aondoke, hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu, hadi chumbani kwake yule aliyenizaa. Biblia Habari Njema - BHND Mara tu nilipoachana nao, nilimwona mpenzi wangu wa moyo; nikamshika wala sikumwachia aondoke, hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu, hadi chumbani kwake yule aliyenizaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mara tu nilipoachana nao, nilimwona mpenzi wangu wa moyo; nikamshika wala sikumwachia aondoke, hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu, hadi chumbani kwake yule aliyenizaa. Neno: Bibilia Takatifu Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita nilimpata yule moyo wangu umpendaye. Nilimshika na sikumwachia aende hadi nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. Neno: Maandiko Matakatifu Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita nilimpata yule moyo wangu umpendaye. Nilimshika na sikumwachia aende mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. BIBLIA KISWAHILI Kitambo kidogo tu nilipoachana nao, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. |
Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?
Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungi yake.
Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha; Ningekunywesha divai iliyokolea, Divai mpya ya mkomamanga wangu.
Sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya giza; sikuwaambia wazao wa Yakobo; Nitafuteni bure; Mimi, BWANA, nasema ukweli; nanena mambo ya haki.
Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.