Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?
Wimbo Ulio Bora 3:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walinzi wa mji waliniona walipokuwa wanazunguka mjini. Basi nikawauliza, “Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?” Biblia Habari Njema - BHND Walinzi wa mji waliniona walipokuwa wanazunguka mjini. Basi nikawauliza, “Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walinzi wa mji waliniona walipokuwa wanazunguka mjini. Basi nikawauliza, “Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?” Neno: Bibilia Takatifu Walinzi walinikuta walipokuwa wakizunguka mji. Nikawauliza, “Je, mmemwona yule moyo wangu umpendaye?” Neno: Maandiko Matakatifu Walinzi walinikuta walipokuwa wakizunguka mji. Nikawauliza, “Je, mmemwona yule moyo wangu umpendaye?” BIBLIA KISWAHILI Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? |
Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?
Walinzi wazungukao mjini waliniona, Wakanipiga na kunitia jeraha, Walinzi walindao kuta zake Wakaninyang'anya shela yangu.
Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;
Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu.
Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi.