Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Wimbo Ulio Bora 3:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliamka nikazunguka mjini, barabarani na hata vichochoroni, nikimtafuta yule wangu wa moyo. Nilimtafuta, lakini sikumpata. Biblia Habari Njema - BHND Niliamka nikazunguka mjini, barabarani na hata vichochoroni, nikimtafuta yule wangu wa moyo. Nilimtafuta, lakini sikumpata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliamka nikazunguka mjini, barabarani na hata vichochoroni, nikimtafuta yule wangu wa moyo. Nilimtafuta, lakini sikumpata. Neno: Bibilia Takatifu Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata. Neno: Maandiko Matakatifu Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata. BIBLIA KISWAHILI Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. |
Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?
Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondosha manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.
Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu.
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu uko karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.