Wimbo Ulio Bora 3:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usiku kitandani nilimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nilimtafuta, nisimpate. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata. Biblia Habari Njema - BHND Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata. Neno: Bibilia Takatifu Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata. Neno: Maandiko Matakatifu Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata. BIBLIA KISWAHILI Usiku kitandani nilimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nilimtafuta, nisimpate. |
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?
Nilimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.
Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.
Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,