Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 2:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nishibishe na zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, maana naugua kwa mapenzi!

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nishibishe na zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, maana naugua kwa mapenzi!

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nishibishe na zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, maana naugua kwa mapenzi!

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Wimbo Ulio Bora 2:5
14 Marejeleo ya Msalaba  

Akawagawia watu wote, mkutano wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake.

Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.

Nafsi yangu inaambatana nawe sana; Mkono wako wa kulia unanitegemeza.

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.

Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Matiti yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera;

BWANA akaniambia, Nenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile BWANA awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.

Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia Maandiko?

Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;