Wimbo Ulio Bora 1:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe ee mpenzi wangu, nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao. Biblia Habari Njema - BHND Wewe ee mpenzi wangu, nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe ee mpenzi wangu, nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao. Neno: Bibilia Takatifu Mpendwa wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao. Neno: Maandiko Matakatifu Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao. BIBLIA KISWAHILI Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao. |
Nao farasi aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi, kila kundi na thamani yake.
Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua, Nyuma ya barakoa yako. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.
Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza, Mwenye kupendeza kama Yerusalemu, Wa kutisha kama jeshi lenye bendera.
Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!