Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi.
Wimbo Ulio Bora 1:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema mierezi itakuwa nguzo za nyumba yetu, na miberoshi itakuwa dari yake. Biblia Habari Njema - BHND mierezi itakuwa nguzo za nyumba yetu, na miberoshi itakuwa dari yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza mierezi itakuwa nguzo za nyumba yetu, na miberoshi itakuwa dari yake. Neno: Bibilia Takatifu Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, na mapao yetu ni miberoshi. Neno: Maandiko Matakatifu Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, na mapao yetu ni miberoshi. BIBLIA KISWAHILI Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi. |
Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi.
Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi.
Nayo nyumba kubwa ilizungushiwa miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, juu yake akaichora mitende na minyororo.
Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungi yake.
Kama akiwa tu ukuta, Tumjengee buruji za fedha; Na kama akiwa ni mlango, Tumhifadhi kwa mbao za mierezi.
Asemaye, Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.
na vizingiti, na madirisha yaliyofungwa, na baraza za pande zote za ghorofa zile tatu, zilizokikabili kizingiti, zilitiwa mabamba ya mti pande zote; na toka chini hadi madirishani; (nayo madirisha yamefunikwa);
Kukabili zile dhiraa ishirini za ua wa ndani, na kukabili sakafu ya mawe ya ua wa nje, palikuwa na baraza kukabili baraza katika ghorofa ya tatu.