Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.
Wimbo Ulio Bora 1:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakika u mzuri ewe nikupendaye, u mzuri kweli! Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu; Biblia Habari Njema - BHND Hakika u mzuri ewe nikupendaye, u mzuri kweli! Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakika u mzuri ewe nikupendaye, u mzuri kweli! Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu; Neno: Bibilia Takatifu Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, tazama jinsi unavyopendeza! Na kitanda chetu ni cha majani mazuri. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, tazama jinsi unavyopendeza! Na kitanda chetu ni cha majani mazuri. BIBLIA KISWAHILI Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani; |
Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.
Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Niliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu.
Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani.
Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondosha manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.
Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.