Mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nilimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
Waroma 4:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, tusemeje juu ya Abrahamu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tuseme nini basi, juu ya Abrahamu baba yetu? Biblia Habari Njema - BHND Tuseme nini basi, juu ya Abrahamu baba yetu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tuseme nini basi, juu ya Abrahamu baba yetu? Neno: Bibilia Takatifu Tuseme nini basi, kuhusu Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili: yeye alipataje kujua jambo hili? Neno: Maandiko Matakatifu Tuseme nini basi, kuhusu Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili: yeye alipataje kujua jambo hili? BIBLIA KISWAHILI Basi, tusemeje juu ya Abrahamu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? |
Mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nilimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto.
Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Abrahamu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wowote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
Wewe u mkuu kuliko baba yetu Abrahamu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Abrahamu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Abrahamu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.
Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)
Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazawa wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Abrahamu; aliye baba yetu sisi sote;
Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? La hasha! Lakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia. Wao ni uzao wa Abrahamu? Na mimi pia.
Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?