Waroma 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC La hasha! Mungu aonekane kuwa kweli japo kila mtu ni mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulikane kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima, ingawaje kila binadamu ni mwongo. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Kila usemapo, maneno yako ni ya kweli; na katika hukumu, wewe hushinda.” Biblia Habari Njema - BHND Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima, ingawaje kila binadamu ni mwongo. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Kila usemapo, maneno yako ni ya kweli; na katika hukumu, wewe hushinda.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima, ingawaje kila binadamu ni mwongo. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Kila usemapo, maneno yako ni ya kweli; na katika hukumu, wewe hushinda.” Neno: Bibilia Takatifu La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa: “Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena, na ukashinde unapotoa hukumu.” Neno: Maandiko Matakatifu La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa: “Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena, na ukashinde utoapo hukumu.” BIBLIA KISWAHILI La hasha! Mungu aonekane kuwa kweli japo kila mtu ni mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulikane kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu. |
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, na jina lako juu ya vyote.
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Waliposikia hayo walisema, Hasha! Yasitukie haya!
Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? La hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazawa wa Abrahamu, mtu wa kabila la Benyamini.
Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? La hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.
Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? La hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? La hasha!
Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? La hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.
Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? La hasha! Lakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? La hasha!
Lakini ikiwa sisi wenyewe, kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha!
Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure.
Lakini mimi, la hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.