Waroma 3:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Myahudi ana nini zaidi? Na kutahiriwa kwafaa nini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watu wengine? Au kutahiriwa kuna faida gani? Biblia Habari Njema - BHND Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watu wengine? Au kutahiriwa kuna faida gani? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watu wengine? Au kutahiriwa kuna faida gani? Neno: Bibilia Takatifu Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? Neno: Maandiko Matakatifu Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? BIBLIA KISWAHILI Basi Myahudi ana nini zaidi? Na kutahiriwa kwafaa nini? |
Kwa maana mwenye hekima hupata faida gani kuliko mpumbavu? Au maskini ana nini kuliko yeye ajuaye kwenda mbele ya walio hai?
Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi?
Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wagiriki ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;
Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nilipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.
Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida.