Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Priskila na Akila walipomsikia wakampeleka kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Waroma 16:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Wasalimuni Prisila na Akila, watumishi wenzangu katika Al-Masihi Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Wasalimuni Prisila na Akila, watumishi wenzangu katika Al-Masihi Isa. BIBLIA KISWAHILI Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; |
Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Priskila na Akila walipomsikia wakampeleka kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo.
waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao.
Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.
Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.
Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
Lakini niliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mfanyakazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
Na Yesu aitwaye Yusto awasalimu. Hao tu ndio watu wa tohara miongoni mwa wale watendao kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada kwangu.