Waroma 14:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani, na yanayotusaidia kujengana. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani, na yanayotusaidia kujengana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani, na yanayotusaidia kujengana. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo na tufanye bidii kutafuta yale yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo na tufanye bidii kutafuta yale yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi. BIBLIA KISWAHILI Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. |
Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.
Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
Na kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga.
Mnadhani hata sasa ya kuwa najitetea kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo.
Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;