Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Waroma 14:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mwenyezi Mungu. BIBLIA KISWAHILI Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. |
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena.
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee malipo ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, yawe ni mema au mabaya.