Waroma 1:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine. Biblia Habari Njema - BHND hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine. Neno: Bibilia Takatifu wajinga, wasioamini, wasio na huruma na wakatili. Neno: Maandiko Matakatifu wajinga, wasioamini, wasio na huruma na wakatili. BIBLIA KISWAHILI wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; |
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Njia kuu zimeachwa, msafiri ameikimbia barabara; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,