Walawi 8:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe, akawaosha kwa maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo Mose akawaleta Aroni na wanawe na kuwatawadha. Biblia Habari Njema - BHND Hapo Mose akawaleta Aroni na wanawe na kuwatawadha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo Mose akawaleta Aroni na wanawe na kuwatawadha. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Musa akamleta Haruni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Musa akamleta Haruni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji. BIBLIA KISWAHILI Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe, akawaosha kwa maji. |
hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike, kumteketezea BWANA sadaka ya moto;
Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.
Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni kutoka kwa uchafu wenu wote, na kutoka kwa vinyago vyenu vyote.
Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa.
Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi ya kuwatakasa kutoka kwa dhambi na kwa unajisi.
Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.
kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kunawa kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.