Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.
Walawi 8:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nacho kitakachosalia katika hiyo nyama na mikate mtakichoma moto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyama yoyote au mkate wowote utakaosalia ni lazima kuteketezwa. Biblia Habari Njema - BHND Nyama yoyote au mkate wowote utakaosalia ni lazima kuteketezwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyama yoyote au mkate wowote utakaosalia ni lazima kuteketezwa. Neno: Bibilia Takatifu Kisha mteketeze nyama na mikate iliyobaki. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki. BIBLIA KISWAHILI Nacho kitakachosalia katika hiyo nyama na mikate mtakichoma moto. |
Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.
Na kwamba kitu chochote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au chochote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
lakini hicho kitakachosalia, katika hizo nyama za sadaka, hata siku ya tatu kitachomwa moto.
Wala msitoke nje mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba, hadi siku za kuwekwa wakfu kwenu zitakapotimia; kwa kuwa atawaweka muda wa siku saba.
(Kwa maana asema, Kwa wakati uliokubalika nilikusikia, Na katika siku ya wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)