Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Walawi 7:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mguu wa nyuma wa upande wa kulia mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka kwa hizo sadaka zenu za amani.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mguu wa kulia wa nyuma wa mnyama wa sadaka zenu za amani mtampa kuhani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mguu wa kulia wa nyuma wa mnyama wa sadaka zenu za amani mtampa kuhani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mguu wa kulia wa nyuma wa mnyama wa sadaka zenu za amani mtampa kuhani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mguu wa nyuma wa upande wa kulia mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka kwa hizo sadaka zenu za amani.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Walawi 7:32
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe;


Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.


Kati ya wana wa Haruni, huyo atakayeisongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake, yeye atapata mguu wa nyuma wa upande wa kulia kuwa sehemu yake.


Kwa maana, hicho kidari cha kutikiswa, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.


na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza.


Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyovileta kwa kuhani, vitakuwa ni vyake.


naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa; kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai.


Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.


Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa kando ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hadi wakati uliokusudiwa, maana nilisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.