Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.
Walawi 7:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu yeyote alaye damu, mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.” Biblia Habari Njema - BHND Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.” Neno: Bibilia Takatifu Mtu yeyote atakayekula damu lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa mtu yeyote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ” BIBLIA KISWAHILI Mtu yeyote alaye damu, mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake. |
Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.
Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake.
Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
Ndipo wakamwambia Sauli, wakisema, Angalia, watu hao wanakosa juu ya BWANA, kwa jinsi wanavyokula pamoja na damu. Naye akasema, Ninyi mmefanya kwa hiana; vingirisheni kwangu leo jiwe kubwa.